Kuhusu Sisi

Ili kuyafanya maisha yako kuwa mazuri unayakiwa kuwajibika kujifunza kutokana na kila changamoto na vikwazo. Zanzibar Learning 4 Life Foundation (ZL4LF) ni taasisi isiyo ya kiserikali inayosaidia vijana kukamilisha malengo yao ambayo kwa kawaida inaonekanwa ni vigumu kufikiwa. Tunasisitiza suala zima la mawasiliano hasa ujuzi katika lugha na vilevile uvumilivu katika maendeleo binafsi.

ZL4LF (iliyojulikana kama PLCI) inafanya kazi na watu duniani kote ambao huchangia mawazo katika kuboresha maisha. Tunatoa elimu endelevu na mafunzo ya amali kwa lengo la kutoa njia mbadala katika kupambana na tatizo la ukosefu wa ajira nchini bila ya kujali jinsia na utashi wa kidini.

Tunatoa mafunzo ya kiingereza, kijerumani, kifaransa, computer na hisabati. Kama unahitaji kujiunga na madarasa yetu tafadhali wasiliana nasi katika zanzibarl4lf@gmail.com au piga simu nambari +255 (0) 773 110 738 au fika katika kituo chetu kilichopo Fuoni Melitato Msikitini.

ZL4LF ilianzishwa mwaka 2006 na Gasica (Shafii Mwita Haji) kijana wa kizanzibari. Taasisi ilianza kwa idadi ndogo ya wanafunzi na kuzidi kukua hadi sasa ina zaidi ya wanafunzi 300.

Swimming.jpg